𝟏. 𝐊𝐔𝐖𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐎𝐍𝐎 𝐓𝐇𝐀𝐁𝐈𝐓𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐌𝐀𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐊𝐎..
Wewe ni zaidi ya mpishi na Mzaa watoto. Wewe upo duniani kwa kusudi maalum. Nini maono yako, ni Yapi malengo yako? Ni nini sababu ya kuwepo kwako duniani? Je, unataka kumaliza bila kutimiza malengo yako duniani kwa sababu ya ndoa?
Ndoa yako isitie hatarini maono na malengo yako badala yake inapaswa kuchangia katika kuyafanya yawe ukweli na kufanikiwa...
𝟐. 𝐊𝐔𝐖𝐀 𝐍𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐀𝐓𝐎...
Kama huna kazi au biashara unayofanya na unatafuta mwanaume wa ATM wa kutegemea kifedha, utaishia kuwa tegemezi, si mke, Utakuwa mnyonyaji, si mtu anayetoa msaada kama biblia ilivyosema "Akamfanyia msaidizi"
Utakuwa mwanamke aliyekosa thamani, utakuwa ni mzigo, utapelekeshwa utatukanwa wewe pamoja na familia yako mtaonekana ukoo wenu mnalia shida kila kukicha na usisahau kuwa "Chochote kinachotolewa bila heshima basi hakina thamani"
𝟑. 𝐉𝐈𝐓𝐔𝐍𝐙𝐄 𝐌𝐖𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐎...
Baadhi ya wanawake wana miaka ishirini na wanakaribia kufa, kwa nini? Una watoto wangapi? Kwa nini hauko imara, mwenye afya na mvuto? ..
Kama una matatizo ya afya, mpenzi, omba uponyaji kabla ya kuolewa. Kwa imani utapona...Kama unakula vitu visivyofaa, acha na kula chakula chenye afya. Sukari nyingi, nyama nyekundu, chocolati sio nzuri kwako. Zinakusubiri kuathiri mwili wako baadaye...
Fanya mazoezi Mama mbona kina wema sepetu, kina zari the boss lady kina Lady jaydee mbona hawazeeki mbona wanazaa watoto kama wewe kwanini wewe unachoka hivyo, Jipende mwonekano wako wa njee ndio unamshawishi hata mwanaume kuendelea kukutunza.
Sio mwanaume anatoa hela lakini haoni mabadiliko yoyote zaidi ya kubadirisha misuko ya nywele tu. fanya mazoezi tengeneza shape punguza tumbo jiweke imara mwanaume aone kazi anayoifanya sio kumwagilia maua ambayo yanazidi kukauka kadri yanavyozidi kumwagiliwa
𝟒. 𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐙𝐄 𝐉𝐈𝐍𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐆𝐄𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐔𝐌𝐄....
Huongei na mwanaume kama mfanyakazi wako au rafiki yako wa shule ya msingi. Unazungumza naye kama kichwa chako kwa heshima na taadhima. Wanawake wengi wenye uwezo wa kujihudumia wanashida hapa, wanaona kama mwanaume hana kazi kwasababu wao wanajipa kila kitu wanachotaka lakini yambua Ndoa ni taasisi muhimu kwenye maisha yako inakamilisha maana halisi ya maisha yako hapa duniani
Ikiwa huwezi kumheshimu mwanaume kama Mume na kumtambua kama kiongozi katika mahusiano yenu, usifikirie juu ya ndoa, mpenzi au unaweza kuishia talaka au single mother pekee...
𝟓. 𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐙𝐄 𝐉𝐈𝐍𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐏𝐈𝐊𝐀...
Angalia, wanaume hawachezei matumbo yao. Jifunze kupika aina tofauti za chakula na supu...Jifuze hili mapema sana, Mwanaume kupenda kula chakula ulichopika wewe kwa mikono yako kunaongeza maana ya maisha yako na Umuhimu wako kwenye nyumba unaongezeka hata usipokuwepo atamiss vile radha ya chakula chako inavyokuwaga
..Wanaume wanapenda ujasiri. Watoto wanapenda ujasiri. Kupika aina tofauti za supu/chakula kunafanya mume wako asitoke nyumbani na asiwe na haja ya kutembea katika Migahawa na hotel za kupikia sehemu ambazo vitoto vya farao vinaweza kumvutia na kukunyang'anya!.....
𝟔.𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐙𝐄 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐒𝐔 𝐒𝐄𝐗......
Jifunze jinsi ya kumridhisha mwanaume wako, Sio kupitia vitendo Mungu hajaruhusu kufanya mapenzi nje ya ndoa na amekataza kabisa.
Soma vitabu mbali mbali angalia mafundisho online hudhuria semina za mapenzi mahusiano na ndoa humu ndimo sehemu utajifunza jinsi ya kufanya ngona
Kwanza utaanza kujifunza kwa maneno lakini utaanza kuyafanyia kazi pindi tu ukiingia kwenye ndoa
𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊
✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇
https://whatsapp.com/channel/0029VaDURtaHFxP7IBxQOi36
𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐅𝐄𝐑
𝟏. 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀
𝟐. 𝐒𝐓𝐘𝐋𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐄𝐍𝐄
𝟑 𝐁𝐀𝐑𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐘𝐄 𝐇𝐀𝐉𝐀𝐎𝐋𝐄𝐖𝐀
𝐍𝐁: 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐈 𝐒𝐎𝐅𝐓 𝐂𝐎𝐏𝐘 (𝐄_𝐛𝐨𝐨𝐤𝐬)
𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™



