MARAFIKI WAMEFANYA NDOA KUWA NGUMU ZAIDI


 

Ndoa zimekuwa ngumu sana, ndoa zimeambatana na vilio visivyoisha kila siku


Wataalamu wa mahusiano na mapenzi wanajitahidi sana kufanya kazi yao kuhakikisha ndoa hizi zinakuwa salama

Lakini kila kukicha ndo kwanza hali inazidi kuwa mbaya, mpaka wengine wanaamua kutoingia kabisa kwenye ndoa

Na wengine kuamua kuwa single mothers, Ndoa zimegeuka gereza kila ukikaa unaskia vilio, huzuni, kukata tamaa na kupoteza matumaini

Hamu ya kuingia huko wengi wameishiwa, hakuna sababu yoyote ile wanaoyoona ni ya muhimu kuingia huko

wanaume wameamua kuwa wakipata watoto njee fresh, wimbi la single mothers nalo nimeongezeka, kila mwanamke aloyesoma na kuajiliwa hataki kuolewa

Jamii imepoteza muhimili muhimu sana wa maendeleo muhimili huu ni familia, skuizi familia za mama na mtoto au baba na mtoto ndo zinaongoza kwa wingi kuliko ndoa

Nini kinasababisha haya?, leo nilivyokuwa napita mitandaoni nilikutana na picha hii

Ukiangalia picha hii inaujumbe mzito sana ambao wengine hawawezi kuuona

Kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kuchagua wapenzi sio kwasababu wameona ubora wao au kuwapenda wenyewe

Ila kuna rafiki zao, familia zao, ndugu zao na jamaa zao ambao watawasifia kuwa wamepata wapenzi bora hata kama wao hawaoni ubora huo

Marafiki, mawifi, familia pamoja na wachungaji wamekuwa ndio watu ambao wanaamua nani aingie kwenye ndoa na nani

Mtu akipata mpenzi hata kama yeye anamuona ni sahihi kwake ila kama rafiki zake na mashoga zake hawajampenda na  hawamuelewi yupo radhi kuachana naye au kumkataa

Kuna yale maneno wanakwambia, utaskia sasa mwenyewe yule utampeleka wapi? Hata kutembea naye kwa watu ni aibu, jtaskia mdada mwenyewe  mbaya

Hususani wanawake ndio kabisa anakamati ya washauri akipata mpenzi hata kabla hajamkubalia  anampeleka kwenye kwa mashoga zake wakampe ushauri haangalii kama yeye anampenda au laah ila shoga zake wakimwambia yule ni mwenyewe basi anaingia kwenye mahusiano ila wakimkataa na yeye anamkataa

Jambo hili ndilo lililoongeza vilio kwenye ndoa, Ulimchagua kwasababu marafiki zako wanampenda ila wao hawaendi kuishi naye wewe ndo utaona kila rangi ya mateso ya hiyo ndoa

Ulimchagua kwasababu wamesema ni mzuri japo wewe kigezo cha uzuri kwako kilikua ni cha mwisho ila kwakua wamesema basi ukaamua kuingia kwenye ndoa

Naomba kusema kuwa Kwenye maisha ni wewe tu ndio unajua vigezo muhimu ambavyo mume au mke wako anatakiwa kuwa navyo

Na kila mtu anavyakwake hatufanani, kutumia vigezo vya mwingine kuingia kwenye ndoa yako ni sawa na kutumia funguo ya kitasa lingine kufungulia kitasa chako

My dear hakitafunguka zaidi zaidi utaishia kuhangaika nacho utatumia nguvu nyingi na hakiwezi kufunguka kamwe labda uvunje

Msingi uliotumia kuingia kwenye ndoa ndio msingi ambao unaamua ndoa yenu iwaje, furaha yenu iwe ya kiwango gani, mapenzi yenu yawe ya level gani

Hivyo achana na kamati za ushauri Moyo wako hauendeshwi kwa ushauri unaendeshwa na Hisia pamoja na Uhalisia

𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊

✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇

𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐅𝐄𝐑

𝟏. 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀  

𝟐. 𝐒𝐓𝐘𝐋𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐄𝐍𝐄 

𝟑 𝐁𝐀𝐑𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐘𝐄 𝐇𝐀𝐉𝐀𝐎𝐋𝐄𝐖𝐀  

𝐍𝐁: 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐈 𝐒𝐎𝐅𝐓 𝐂𝐎𝐏𝐘 (𝐄_𝐛𝐨𝐨𝐤𝐬)



𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™
Tags