NDOA NI KAMA GARI

 

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema kuwa yeye anaifananisha Ndoa kama gari 🚙

Akasema kuwa watu wengi sana wanakimbilia kuliendesha hili gari wakiwa hawana ujuzi wowote wala elimu yoyote ile ya kuendesha gari

Akimaanisha kwamba Ndoa ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine, Mtu huwezi kuendesha taasisi kama hauna elimu sahihi juu ya uendeshwaji wa taasisi hiyo

Madhara yake nini, Watu wengi sana kwa kukosa elimu ya Ndoa na mahusiano

Wamejikuta wakishindwa kuchagua ni aina gani ya gari ambalo wana weza kuendesha maana mtu anayeendesha gari la mizigo ni tofauti na anayendesha gari la abiria

Na wengi ambao wanataka kuendesha taasisi hii bila hata ya elimu kidogo juu ya uendeshwaji na usimamizi wa Ndoa na mahusiano wamekuwa wakishindwa na wengine kutoka nduki

Na kwakuwa lengo letu sio kuingia tu kwenye ndoa ila lengo ni kukaa kwenye ndoa na kudumu kwenye mahusiano

Hivyo tujitahidi sana kujifunza kabla na baada ya kuingia kwenye hii taasisi ili isitushinde kuendesha wala tusikose furaha

Maana hii ni taasisi ambayo kwa baadhi ya dini haivunjiki mpaka kifo hivyo kama haujui jinsi ya kukuendesha itakusumbua sana na utapoteza furaha ya maisha

𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊

𝗣𝗔𝗚𝗘 𝗬𝗘𝗧𝗨 𝗜𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗢𝗠𝗢 𝗠𝗭𝗨𝗥𝗜 𝗦𝗔𝗡𝗔 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗜𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗔 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜

✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇

https://whatsapp.com/channel/0029VaDURtaHFxP7IBxQOi36/100

𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲

𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮

𝟬𝟳𝟲𝟰 𝟰𝟵𝟵 𝟲𝟴𝟲

 𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺𝘂 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™

Tags