USIACHE NEEMA IKAPITA KWENYE MAISHA YAKO



 Kuna Muda mwanamke unapata mwanaume anakuja kwenye maisha yako unaona kabisa kuwa anakila sifa ya kuwa baba wa watoto wako Lakini sababu wewe ni mzuri sana unaongeza malingo, unaanza kumzungusha kijana wa watu, unampeleka huku na kule ili akuone wa thamani ila bahati mbaya ni kwamba


unavyokalibia tu kuacha malingo ili umkubalie  naye anaona wewe sio mke wa kuoa alikosea kuchagua anaachana na wewe anaenda kutafuta mwanamke mwingine na anamuoa unabaki hapo unaonyesha malingo ya uzuri wako

Kuna muda mwanaume unakuwa na mwanamke unaona kabisa kuwa huyu mwanamke anajielewa, mwanamke ametulia anasifa zote za kuwa mke ni mwanamke bora kuliko wote uliowai kuwa nao

ila kwasababu wewe ni bingwa wa wanawake na unauwezo wa kumpata mwanamke unaye mtaka basi  unaanza kumdharau na kumletea usupper star mpaka mdada wa watu moyo unakufa na anaamua kukuacha alafu kuna jamaa anamuoa baada ya miezi miwili tu na kwenda naye mbali huko

Kuna muda utaona kazi ambayo ulikuwa na vigezo vyote vya kuipata haujaipata kwasababu tu haukufanya juhudi yoyote kwa kuamini utaipata tu ni yako hakuna wa kuipata zaidi yako.

Kuna muda kwenye maisha unapita mahali unapata wazo la biashara lakini kila ukitaka kuanzisha unajisubirisha kwasababu unajua hakuna wa kufanya hiyo biashara zaidi yako lakini kuna siku unapita sehemu ile ile unakuta kuna mtu kafungua biashara ile ile kama uliyokuwa unaifikiria tena ni kubwa kuliko uliyokuwa umeifikiria wewe

Nachotaka kusema ni kwamba kwenye  maisha ya kila  mwanadamu kuna neema ya Mungu lakini neema hii huwa inaexpiredate neema ya Mungu haipogo daima na wewe, haikusubili wewe kama ukishindwa kujua kama sasa nipo kwenye neema basi utaipoteza

Kuna muda kwenye maisha unajikuta umepoteza kile ambacho uliona kabisa ubora wake, uliona uzuri wake, uliona faida zake za kukifanya mapema ila ukaweka kiburi  ukaweka jeuri ukajipa moyo kwamba hakina mahali pakwenda wewe ndio mmiliki.

Wewe utakuwa shahidi kuna vipindi kwenye maisha yako vilikuja mpaka leo ukikaa unajisemea yaani kipindi kile nisingefanyaga vile ningekuwa pale

Yaani kipindi kile nisingemuachaga yule kaka ningekuwaga kwenye ndoa saizi

Yaani kipindi kile ningeanzishaga ile biashara ningekuwa na maisha yenye unafuu sasa lakini neema uliacha ikapita

Nataka nikwambie haujachelewa kwa kuwa Mungu ni wa neema na neema yake haiishi basi amini Ujumbee huu ni Neema kutoka kwake

Ujumbe huu umekuja kukuamsha kukwambia kuwa Pindi neema ya Mungu ikikutembelea basi hakikisha unaifanyia kazi Ukiacha ipotee utaisbi maisha muda mrefu sana bila kukutana nayo tena

Na kwa neema ya Mungu Wewe kama mdau wa Olenga love hub Unaenda kushare ujumbe huu ili Neema hii isiwapite wapendwa wetu

𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊

✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇

𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐅𝐄𝐑

𝟏. 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀  

𝟐. 𝐒𝐓𝐘𝐋𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐄𝐍𝐄 

𝟑 𝐁𝐀𝐑𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐘𝐄 𝐇𝐀𝐉𝐀𝐎𝐋𝐄𝐖𝐀  

𝐍𝐁: 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐈 𝐒𝐎𝐅𝐓 𝐂𝐎𝐏𝐘 (𝐄_𝐛𝐨𝐨𝐤𝐬)




𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™
Tags