Nilikutana nae mara ya kwanza ndani ya Bajaji
Nikamuomba namba ya simu baada ya salamu na maongezi akanipa.
Tulipoachana nikampigia simu nikamueleza kuwa nampenda.Baada ya mvutano wa siku nyingi hatimaye akanikubalia ombi langu.
Siku zilivyoenda nikashangaa haniombi hela wakati ananitembelea umbali mrefu kwa nauli yake kuja kuniona.
Siku moja akanitumia ujumbe kwa Mara ya kwanza akasema-:
"Baby nina shida na shilingi 15,000/= nahitaji kwenda saluni wiki ijayo nimeona nikujulishe mapema ili ujiandae taratibu"
Kwakuwapesa nilikuwa nayo na sio kawaida yake kuniomba nikazama mfukoni nikamtumia 50,000/= kwenye namba yake akanijibu-:
"Baby asante nimepata ila nimekuomba 15,000/= inanitosha nakurudishia 35,000/= iliyobakia ili uendelee kuizungusha kwenye biashara itusaidie wote hapo baadae"
Kabla sijamkatalia kurudisha hela ujumbe ukaingia kwenye simu yangu kuwa nimepokea 35,000/= toka kwa Catherine.
Nilishikwa na mshangao aliponiambia anahamu ya kukutana na Mimi maana tokea tufahamiane sijawahi kumhitaji faragha kwa hiyo 10,000/= inamtosha saluni na 5,000/= atatumia kwa nauli ya kuja kwangu na kurudi kwao.
Wakati najiandaa kumpa ratiba ya mtoko ghafla nikatoka kwenye ndoto hii ya ajabu.
SWALI LANGU
JEE WANAWAKE WA AINA HII WAPO KWELI KWA SASA????
𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊
𝗣𝗔𝗚𝗘 𝗬𝗘𝗧𝗨 𝗜𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗢𝗠𝗢 𝗠𝗭𝗨𝗥𝗜 𝗦𝗔𝗡𝗔 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗜𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗔 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜
✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇
https://whatsapp.com/channel/0029VaDURtaHFxP7IBxQOi36/100
𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝟬𝟳𝟲𝟰 𝟰𝟵𝟵 𝟲𝟴𝟲
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™



