Mwanamke jua wewe ni Namba ngapi na Mwanaume jua mke wako anaangukia kundi gani
1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia
kulia tuu!
2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa
muda wote hadi ikukere!
3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna,
haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano
kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!
4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla
ghafla inafuata!
5. Wako wanawake ambao, akichukia,
Atakachokishika usipokimbia anakutandika na
anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye!
6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake
zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa
nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na
watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa
kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!
7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana
kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama
yoote!
8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga
mabegi na kuondoka!
9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!
10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala
kimyaaa!!
11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo
linakata, na pengine mpaka wanaharisha!
13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia
kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa.
Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda
sokoni.
14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka
saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii
ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru
kiurahisi.
15 Kuna wale ambao yeye akiwa na hasira anatafuta earphone au anawasha Muziki kisha anaweka sauti hadi mwisho, Siku hiyo ni kuskiliza muziki mwanzo mwisho hawa huchanganya na kutoongea na mtu yeyote zaidi ya kujiimbia tu
𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊
𝗣𝗔𝗚𝗘 𝗬𝗘𝗧𝗨 𝗜𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗢𝗠𝗢 𝗠𝗭𝗨𝗥𝗜 𝗦𝗔𝗡𝗔 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗜𝗟𝗜 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗔 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜
✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇
https://whatsapp.com/channel/0029VaDURtaHFxP7IBxQOi36/100
𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝟬𝟳𝟲𝟰 𝟰𝟵𝟵 𝟲𝟴𝟲
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺𝘂 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™


