UNALINGIA NINI?


Kesho inaweza ikawa jana tukifika kesho kutwa, ila jana haiwezi kuwa kesho maadam tushaipita. Huenda tuna vitu vingi sana vya kuviogopa duniani, ila tafadhali ni bora tuogope zaidi kwamba tunaishi halafu tunaishia.

Hadithi za muda huwa ni mithili ya upepo upukutishao vumbi. Ni suala la kufumba na kufumbua kisha kila kitu huwa kimepotea.

Yule mwali aliekuwa akivimba sababu ya uzuri wake hivi sasa kawa bibi, kila kitu chake kimeshuka yote ni kwa sababu leo sio jana.

Hata yule Handsome aliyejiona yeye ni yeye, leo kawa babu hana tena attention mbele za watu. Ama kweli wahenga hawakukosea waliposema "kila mfalme na zama zake"

Kiburi chako na majivuno ni ndoto tu katika ardhi ya upotevu, jua la muda likikucha basi utakuja kujua kuwa ulikuwa hujui kwamba hujui. "Wewe si chochote mbele ya muda .."

Dunia inapita na kila kitu chake kinapita, hivyo nikuulize muungwana umeamua kuringa na nini kwenye uso wa dunia hii ya mpito. Je, na mali, fedha, au na uzuri wako. Mbona unasita kunijibu ?? "hakika Mheshimu Mungu kisha uogope sana Muda"

Kinachosikitisha ni kwamba, tunaweza tazama kalenda ya nyuma, ila kamwe hatuwezi kurudi nyuma. Kadri muda unavyosonga ndivyo ambayo kila kitu juu ya dunia hii nacho kinasonga.

Kabla ya wewe kuwepo kwenye uso wa dunia hii walikuwepo wababe kukuzidi wewe, wazuri kuliko wewe, wenye kila shauku ya ushawishi mbele ya wawatazamao ila nao wamepita kama kivuli zimebaki tu hadithi zao. "This time tomorrow is passed like a shadow"

Kila kitu kwenye uso wa dunia hii ni kama umande tu, daima haudumu. Hivyo kaa chini tafakari na ujiulize wewe binafsi umeamua kuwekeza kwenye nini. Ikiwa ni kwenye majivuno ya uzuri wako, basi subiri hadi pale utakapoona dimpozi za uso wako zikiwa makunyanzi ya uzee wako.

Kuna maisha baada ya leo 🙌🏽

Wala sikutishi ila lazima utambue kuna maisha baada ya leo. Matendo mema, haiba safi na utu, ni bora kuliko kujitia kutu na kujiona Mungu mtu. Nakukumbusha tu, "ukiona tunda limeiva, basi ujue hata kuoza pia limekaribia"

𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊

✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇 

 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐅𝐄𝐑

𝟏. 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀   

𝟐. 𝐒𝐓𝐘𝐋𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐄𝐍𝐄
  
𝟑 𝐁𝐀𝐑𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐘𝐄 𝐇𝐀𝐉𝐀𝐎𝐋𝐄𝐖𝐀   
𝐍𝐁: 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐈 𝐒𝐎𝐅𝐓 𝐂𝐎𝐏𝐘 (𝐄_𝐛𝐨𝐨𝐤𝐬)


 𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲 
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮 
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™