Kuna watu wengi sana hawajui kuwa kunabadhi ya watu na madhehebu yapo kwaajili ya kununua imani na hii ni kwasababu watu wengi hawajui kuwa imani ni sawa na kito cha thamani imani inafananishwa na dhahabu, almasi na madini mengine
Kazi ya kununua imani ilianza toka zamani sana Mfano wa kwanza nitakupa pale Shetani alipo Kuwa akimjaribu Yesu kule jangwani Alimjaribu kwa vitu vingi lakini alipo taka kuipata imani yake alimwamwonyesha milki kubwa zenye utajiri wa kila aina kisha akamwambia ukinisujudia milki hizi zote zitakuwa zako
.....swali la kujiuliza kwanini kitendo kidogo tu cha kusujudu kimpe mtu utajiri wa milki kubwa kama zile? hii ni kwasababu mabadilishano ya imani na zile milki zote yalikuwa yanalenga kuipata imani maana imani inathamani kuliko zile milki zote
Watu wengi hawajui kuwa imani ni kitu chenye thamani isiyofananishwa na kitu chochote kile ndomana kuna watu wapo tayari kukupa chochote unachotaka ili mradi usujudu kwenye madhabahu ambazo wao wanazisujudu
Na hapa shida sio wao shida ni wewe maana wao wanajua wanachokisujudu ila wewe kwakuwa wamekupamba tu kwa maua ya fedha na vitu mbali mbali basi unaona niungane nao hata kama haujui ni nini wanakisujudu mahali hapo
Nachotaka nikwambie ni kwamba wewe unaona fedha na ahadi mbali mbali wanazotoa ni za thamani sana ila ni sawa na kubadilishana dhahabu na Jiwe Maana unachowapa wao ni mara mia bora kuliko wanachokupa wewe japo kwenye ulimwengu wa mwili unaona ni sawa tu ila kwenye ulimwengu wa roho jua kabisa umefanya bogus treaty kama ile aliyofanya chief mangungo msovero
Protect your Faith yeah linda imani yako kwa yesu maana kuna madhehebu mengi sana yanafanya kazi ya kununua imani za watu na sababu kubwa ni umaskini wanawapa pesa kidogo na misaada mbali mbali kisha wanawaingiza kuabudu vitu ambavyo hata ukiuliza hawajui wanaabudu nini
Kitu cha kukumbuka ni kwamba Hatuabudu dini (we dont worshipping religion) tunamuabudu Mungu aliyejidhihirisha kwetu kupitia Mwanawake Yesu kristo
Ukiona mtu yeyote yule anahusisha imani na fedha au utajiri au msaada kaa mbali sana na mtu huyo maana anataka akupe jiwe ili wewe umpe dhahabu
Walimpa yuda vipande vya fedha ili Auze imani yake juu ya Yesu Lakini baada ya yuda kujua alichokipoteza aliona hata vile vipande vingejaa dunia nzima haviwezi kulingana na thamani ya imani aliyoipoteza
Wake up Amka Dunia ni zaidi ya hivi tunavyoviona
𝐃𝐚𝐫𝐚𝐬𝐚 𝐥𝐢𝐦𝐞𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐇𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢
🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊 🎊
✅ 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐎𝐌𝐎 𝐘𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐏𝐈𝐓𝐀 𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 👇👇👇
https://whatsapp.com/channel/0029VaDURtaHFxP7IBxQOi36
𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐅𝐄𝐑
𝟏. 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐍𝐉𝐄 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀
𝟐. 𝐒𝐓𝐘𝐋𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐄𝐍𝐄
𝟑 𝐁𝐀𝐑𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐘𝐄 𝐇𝐀𝐉𝐀𝐎𝐋𝐄𝐖𝐀
𝐍𝐁: 𝐕𝐈𝐓𝐀𝐁𝐔 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐈 𝐒𝐎𝐅𝐓 𝐂𝐎𝐏𝐘 (𝐄_𝐛𝐨𝐨𝐤𝐬)
𝗜𝘁𝘀 𝗺𝗲
𝗠𝗮𝘁𝗵𝗮𝘆𝗼 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮
𝗠𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺 𝘄𝗮 𝐌𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶, 𝐌𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝘆𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮™



